Usawirishaji wa Uhusika katika riwaya za Rosa Mistika na Maisha Kitendawili

Authors

  • Shadrack Tete Muia Department of Linguistics and Languages, Machakos University, Kenya
  • John Mutua Department of Linguistics and Languages, Machakos University, Kenya
  • Vifu Makoti Department of Linguistics and Languages, Machakos University, Kenya

Keywords:

fani, mbinu, mtindo, sanaa, uhusika, usawiri, wahusika

Abstract

Makala hii inajadili usawirishaji wa uhusika katika riwaya za Rosa Mistika na Maisha Kitendawili. Kipengele cha wahusika ni muhimu katika kazi ya fasihi kwani hushirikiana na vipengele vingine vya fani ili kutoa ujumbe wa kazi ya fasihi. Kwa kawaida wahusika hujengwa kisanaa na mwandishi ili waweze kuwasilisha dhana mbalimbali za maisha katika jamii. Kwa hivyo lengo la makala hii ni kuchambua uwashirishaji wa wahusika wakuu katika riwaya za Rosa Mistika ya Euphrase Kezilahabi na Maisha Kitendawili ya John Habwe Kwa kawaida wahusika hujengwa kisanaa na mwandishi ili waweze kuwasilisha dhana mbalimbali za maisha katika jamii. Kipengele cha wahusika ni muhimu katika kazi ya fasihi kwani hushirikiana na vipengele vingine vya fani ili kutoa ujumbe wa kazi ya fasihi. Mwandishi huwajenga wahusika wake kwa kutumia mbinu mbalimbali ili kuwatofautisha na kuiwezesha hadhira yake kutambua sifa za mhusika fulani na kutofautisha na mhusika mwingine katika kazi ya fasihi. Kwa hivyo lengo la makala hii ni kubainisha mfanano wa wahusika wakuu katika riwaya za Rosa Mistika (Euphrase Kezilahabi) na Maisha Kitendawili (John Habwe). Ili kufikia lengo la makala hii tumeongozwa na nadharia ya udhanaishi. Nadharia hii imetuwezesha kubainisha sifa za wahusika wakuu kama zilivyosawiriwa na waandishi.

Dimensions

Euphrase, K. (1971). Rosa Mistika. Nairobi. Kenya Litrature Bureau.

Habwe, J. (2000). Maisha Kitendawili. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation.

Msokile, M. (1992). Misingi ya Hadithi Fupi. Dar-es- Salaam University Press.

Njogu, K., & Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Senkoro, F. M. K. (1987). Fasihi na Jamii. Dar-es- salaam: Press and Publicity Centre.

Wamitila, K.W. (2002). Uhakiki wa Fasihi. Misingi na Vipengele vyake. Nairobi: Phoenix Publishers L.t.d.

_________(2003). Kamusi ya Fasihi, Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publishers.

_________ (2008). Misingi ya Uchambuzi wa Fasihi. Nairobi. Vide Mulwa Publishers L.t.d.

Wafula, R., & Njogu, K. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi: Nairobi. Sai Industries Limited.

Wanjala, F. S. (2011). Kitovu cha Fasihi Simulizi kwa Shule, Vyuo na Ndaki. Mwanza : Serengeti Publishers.

Published

2023-02-21

How to Cite

Usawirishaji wa Uhusika katika riwaya za Rosa Mistika na Maisha Kitendawili. (2023). Research Journal in African Languages, 4(2). https://royalliteglobal.com/african-languages/article/view/1053

Issue

Section

Articles

How to Cite

Usawirishaji wa Uhusika katika riwaya za Rosa Mistika na Maisha Kitendawili. (2023). Research Journal in African Languages, 4(2). https://royalliteglobal.com/african-languages/article/view/1053