Filamu za runinga kama chombo kinachomdhalilisha mwanamke wa kiafrika katika asasi ya ndoa

Authors

  • Thedius Bwire Ojiambo Idara ya Kiswahili na Mawasiliano, Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Kijamii, Chuo Kikuu Cha Kikatoliki Cha Afrika Mashariki

Keywords:

Tandavu la Korona; Asasi ya Ndoa; Soap Opera; Walala Hai; Walala Hoi; Madongoporomoka; Bwanyenye

Abstract

Tandavu la Korona, ambalo limefaulu kuzitawisha familia majumbani, limezipa umaarufu filamu katika runinga za Kenya. Makala hii inatathimini filamu ya runinga kama chombo kinachomdhalilisha mwanamke wa Kiafrika katika asasi ya ndoa. Maria, filamu ambayo ilishabikiwa na Wakenya wengi katika TV ya Citizen  ndiyo inayoshughulikiwa. Kwa kutumia nadharia ya ufeministi wa Kiislamu, makala hii inachanganua nafasi ya wahusika wa kike katika kumnasua mwanamke wa Kiafrika kutoka katika minyororo ya asasi ya ndoa ambayo imemtia kifungoni kwa muda mrefu mpaka asiweze kujitegemea. Makala hii imegundua kwamba, katika ndoa nyingi, mwanamke mwafrika ameendelea kusawiriwa kama kiumbe anayemtegemea mwanamme kijamii na kiuchumi. Kwa hivyo, kwa vile ushabikiaji TV unaendelea kuwa na athari kubwa kwa watazamaji, tunapendekeza kuwa ingekuwa bora kama mwanamme na mwanamke wangesawiriwa kama viumbe sawa wanaotegemeana na kuhitajiana katika ndoa.

References

Ahmed, Leila (1992) Women and Gender in Islam. Connecticut: Yale University Press.

Evans, J. (1995) Feminist Theory Today: An Introduction to Second- Wave Feminism. New Park, CA: SAGE Publications.

GeoPoll Survey https://www.geopoll.com

Hussein, E. (1983) “Hatua Mbali Mbali za Kubuni na Kutunga Tamthilia Kufuatana na Misingi ya Ki-Aristotle” Katika Fasihi III Makala za Semina, Dar-es-Salaam.

Kiango, S. D. (1992) Taswira ya Mwanamke katika Tamthiliya za Kiswahili za Kenya Zilizochapishwa,” katika Baragumu Juzuu 1 na 2, Tasinifu ya M.A, Chuo Kikuu cha Maseno. Maseno, Kenya.

Killam, C. D (Mhariri) (1973) African Writers on African Writing Heinemann, London.

Kioko, Mutua K. (2020) Matumizi ya Lugha Kama Kigezo cha Utabaka: Mfano wa Maria katika Runinga ya Citizen, Kazi Mradi Haijachapishwa, Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki, Nairobi.

Lawrence-Hart, Grace (2019) “The Social Cultural Significance of Polygamy in Africa” in Journal of Social Sciences and Humanities, Ignatious Ajuru University, Port Harcout, Rivers State.

Noordin, Mohamed M. (2006) “Nadharia ya Ufeministi wa Kiislamu katika Fasihi ya Kiswahili” katika Nadharia katika Taaluma ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika. Eldoret: Moi University Press

Oyori, O. N. (2006) Nadharia katika Taaluma ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, Moi University Press.

Wafula, R. M. (1999) Uhakiki wa Tamthilia: Historia na Maendeleo Yake Jomo Kenyatta Foundation, Nairobi.

Wafula, R. M. na Njogu, K. (2007) Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Wamitila, K. W (2002) Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake, Phoenix Publishers, Nairobi.

Downloads

Published

2021-09-04

Issue

Section

Articles

How to Cite

Filamu za runinga kama chombo kinachomdhalilisha mwanamke wa kiafrika katika asasi ya ndoa. (2021). Research Journal in African Languages, 2(3). https://royalliteglobal.com/african-languages/article/view/674

Similar Articles

11-20 of 24

You may also start an advanced similarity search for this article.