Matumizi ya taswira katika usawiri wa mashairi ya Euphrase Kezilahabi na Kithaka wa Mberia
Keywords:
Euphrase Kezilahabi Kithaka wa MberiaAbstract
Makala hii imechunguza taswira na viwango vya taswira vinavyotumika katika usawiri wa maudhui ya ukoloni mamboleo na uchumi. Aina mbalimbali za taswira za lugha zimechanganuliwa. Taswira imegawika katika matapo mawili makuu: ishara na maelezo. Wamitila anachanganua zaidi taswira na kuibuka na taswira za uoni, za harufu, za joto, za mguso, za mwonjo na usikivu. Senkoro (1982:37) anatambua makundi matatu makuu ya taswira: zionekanazo, za mawazo na hisi. Taswira zionekanazo ni taswira za kiishara. Taswira za mawazo ni za kidhahania, ilhali taswira za hisi huibua hisi fulani mawazoni. Taswira za hisi hushughulikia mielekeo ya kihisia ya msomaji kuhusu hali fulani. Huweza kumfanya msomaji awe na wasiwasi, aone woga, au apandwe na hasira kwa vile hujihusisha na hisi za ndani. Taswira hizi zina nguvu kubwa ya kuganda akilini na kumwezesha msomaji kuupata ujumbe wa mtunzi vizuri. Kulingana na Senkoro (1982), taswira za hisi huweza pia kujengwa ndani ya tamathali. Utafiti huu ulitumia msingi wa nadharia ya Mtindo ilioasisiwa na Buffon (1930) na kuendelezwa na Leech (1969). Mtindo ni elementi ya kimsingi katika maana ya jumla ya kazi ya fasihi lakini ni kupitia maudhui ndipo maana halisi ya mitindo iliyotafitiwa imeweza kujitokeza. Hauwezi zungumzia mitindo bila kuzungumzia maudhui. Maudhui ya ukoloni mamboleo na uchumi yalitumika katika utafiti kwa vile ni mojawapo ya maudhui yanayoweza kubeba mabadiliko yanayoshamiri katika mitindo ya kishairi. Kwa hivyo, si kwamba maudhui mengine hayangetumika katika utafiti huu. Mashairi yaliyoteuliwa ndiyo yamechunguzwa katika utafiti huu. Mashairi yanayohusu maswala ya ukoloni mamboleo na uchumi yamechanganuliwa kwa kuegemea mihimili ya nadharia ya mtindo. Mihimili ya nadharia hii ya mtindo itatumika kuchanganua ulinganifu na utofauti uliopo katika uasilishaji wa mashairi. Ndiposa ufanano au utofauti uliopo katika kazi za washairi hawa ziweze kudhihirika.
Published
How to Cite
Issue
Section
Copyright (c) 2022 Job Juma

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
This open-access article is distributed under a Creative Commons Attribution (CC-BY) 4.0 license.
You are free to: Share — copy and redistribute the material in any medium or format. Adapt — remix, transform, and build upon the material for any purpose, even commercially. The licensor cannot revoke these freedoms as long as you follow the license terms. Under the following terms: Attribution — You must give appropriate credit, provide a link to the license, and indicate if changes were made. You may do so in any reasonable manner, but not in any way that suggests the licensor endorses you or your use. No additional restrictions You may not apply legal terms or technological measures that legally restrict others from doing anything the license permits.