Udhihirikaji wa mtafsiri katika muktadha wa baadaukoloni

Authors

  • Vincent N. Magugu Department of Kiswahili and Other African Languages, Moi University, Kenya
  • Robert W. Oduori Department of Kiswahili and Other African Languages, Moi University, Kenya
  • Mosol Kandagor Department of Kiswahili and Other African Languages, Moi University, Kenya

Keywords:

Uibuaji ugeni, Tafsiri za Baadaukoloni, Udhihirikaji wa Mtafsiri

Abstract

Maendeleo katika taaluma ya tafsiri mwanzoni mwa miaka ya tisini yalibadilisha mtazamo kuhusu dhana ya tafsiri na kutambua upana na mabadiliko yake. Kupanuka kwa upeo wa taaluma hii kumeeleza na kuumba upya dhima ya mtafsiri. Nafasi ya mtafsiri imebadilika kutoka kwa daraja la kuvusha ujumbe pasi kuuathiri hadi kumtambua mtafsiri kuwa kiungo muhimu kinachoathiri mchakato na zao la tafsiri. Dhana kama vile ulinganifu, uaminifu pamoja na uhakiki wa ubora ambazo awali zilikuwa zenye umuhimu mkuu katika taaluma ya tafsiri zimesukumwa pembeni huku vipengele visivyokuwa vya kiisimu vikitiliwa mkazo. Ufasili na utafsiri wa matini ambao awali ulikuwa mchakato wa kiisimu na kimatini umebadilika na kujiegemeza zaidi kwa vipengele vya kitamaduni na vipengele nje ya isimu. Hali hii ni kweli tunapodhukuru tafsiri za fasihi katika muktadha wa baadaukoloni. Mtafsiri anadhihirika bayana kupitia kwa uteuzi wa kimakusudi ambao unajiegemeza kwa mikakati ya uibuaji ugeni hasa katika kushughulikia vipengele vinavyofungamana na utamaduni chanzi. Mikakati hii inaibua lugha mesto ambayo inahusiana kwa karibu na dhana ya utofauti wa kiisimu na kitamaduni katika mazingira ya baadaukoloni. Kwa kuchunguza tafsiri ya riwaya ya Caitaani Mutharaba-ini ya Ngugi wa Thiong’o kwa Kiingereza, Makala hii imejadili jinsi matini tafsiri imegeuzwa kuwa jukwaa la kukabiliana na ubabe wa kibepari katika ngazi ya isimu na utamaduni pamoja na jinsi udhihirikaji wa mtafsiri unavyobainika kupitia kwa kuchunguza uteuzi wa kimakusudi wa kiisimu ambao mtafsiri alifanya.

References

Alvarez, R.& Vidal, C. (1996). Translation, Power, Subversion. Clevedon /Philadelphia: Multilingual Matters.

Baker, M. (1992). In Other Words: a coursebook on translation. London: Routeledge.

Bandia, P. F. (2008). Translation as Reparation: Writing and Translation in Postcolonial Africa. Manchester: St. Jerome Publishing.

Bandia, P. F. (2010). “Postcolonial Literatures and Translation.” In. Gambier, Y & Doorslaer, L (Eds). Handbook of Translation Studies. (Vol. 1)

Bandia, P. F. (2014). Translation as Reparation: Writing and Translation in Postcolonial Africa. New York: Routledge

Catford, J.C. (1965). A Linguistic Theory of Translation. Oxford: Oxford University Press.

Cook, D. & Okenimkpe, M. (1997). Ngũgĩ: An Exploration of His Writings. (2nd Ed). New Hampshire: Heinemann

Cronin, M. (2003). Translation and globalization. London: Routledge.

Cronin, M. (2006). Translation and identity. London: Routledge.

Holmes, J. (1972): The Name and Nature of Translation Studies, unpublished manuscript, Amsterdam, Translation Studies section, Department of General Studies, reprinted in Toury, G. (ed.) (1987): Translation Across Cultures, New Delhi, Bahri Publications.

Marais, K (2018) A (Bio)Semiotic Theory of Translation: The Emergence of Social-Cultural Reality. London/New York: Routledge

Marais, K (2014) Translation Theory and Development Studies: A Complexity Theory Approach. London/New York: Routledge

Nida, E. A. (1964). Towards a Science of Translating: With Special Reference to Principles and Procedures Involved in Bible Translating. Leiden: Brill.

Ngugi, T. (1986). Decolonizing the Mind: The politics of Language in African literature. Nairobi: East African Educational Publishers.

Ngugi, T. (1981). Detained: A writer’s prison diary. Nairobi: East African Educational Publishers.

Nord, C. (1990). Functionalism and loyalty: some considerations around the translation of titles. Proceedings of the II Complutense Meetings on Translation, 153-162.

Reiss, K na Vermeer, J (1984). Towards a General Theory of Translational Action Skopos Theory Explained. Manchester: St. Jerome Publishing

Shirinzadeh, S.A & Mahadi T.S (2014). “Translating Proper Nouns: A Case study of English Translation of Hafez’s Lyrics. In. English Language Teaching. Vol 7, No. 7. Canadian Centre of Science and Education.

Snell-Hornby, M (2006). The turns of translation studies. New paradigms or shifting viewpoints? Amsterdam: John Benjamins.

Toury, G (1995). Descriptive Translation Studies and Beyond. Amsterdam / Philadelphia: John Benjamins Publishing Company

Tymoczko, M. and Gentzler, E. (2002). Translation and power. Amherst: University of Massachusetts Press

Venuti, L. (1995). The Translator’s Invisibility: A History of Translation. London & New York: Routledge.

Venuti, L. (2008). The Translator’s Invisibility: A History of Translation (2nd ed). London & New York: Routledge.

Williams, J. & Chesterman R. (2002). The Map: A Beginners Guide to Doing Research in Tarnslation Studies. Manchester: St. Jerome.

Zaja, O.J. (2011). Siting, Text, Culture, Context and Pedagogy in Literary Translation: A Theorization of Translation in Cultural Transfer with Examples from Selected Texts in Kiswahili. Unpublished PhD thesis. Kenyatta University

Downloads

Published

2022-03-11

Issue

Section

Articles

How to Cite

Udhihirikaji wa mtafsiri katika muktadha wa baadaukoloni. (2022). Research Journal in African Languages, 3(1). https://royalliteglobal.com/african-languages/article/view/744