Uhusiano wa Lugha na Tabaka: Uchanganuzi wa Riwaya za Kuli na Pendo la Karaha

Main Article Content

Virginia Wambui Mwathi
Vifu Makoti
John Mutua

Abstract

Makala hii inachunguza uhusiano uliopo kati ya lugha na tabaka kwa mujibu wa riwaya za Kuli (Shafi, 1979) na Pendo la Karaha (Habwe, 2014). Lugha ina jukumu muhimu katika jamii ambalo ni kufanikisha mawasiliano; hutumika kuwasilisha habari na hisia za watu. Kando na kuwa chombo cha mawasiliano, lugha hutambulisha: eneo atokalo mtu, cheo chake, na kadhalika. Vilevile, lugha huonyesha mahusiano ni ya aina gani baina ya wazungumzaji, jinsia na tabaka la mzungumzaji. Jamii tuliyomo ina mfumo wa kiuchumi ambao umegawa watu katika matabaka tofauti kulingana na uwezo wao wa kumiliki na kudhibiti njia za uzalishaji mali. Matabaka haya hayakosi kutangamana katika mchakato wa kutafuta riziki. Yanapotangamana, sharti lugha itumike. Kwa hivyo, katika makala hii, tutadadisi aina ya mazungumzo ya mtu ambayo humweka ama katika tabaka la juu au la chini.

Downloads

Download data is not yet available.

Article Details

How to Cite
Mwathi, V. W., Makoti, V., & Mutua, J. (2024). Uhusiano wa Lugha na Tabaka: Uchanganuzi wa Riwaya za Kuli na Pendo la Karaha. Nairobi Journal of Humanities and Social Sciences, 8(1). https://doi.org/10.58256/qkmf2486
Section
Articles

How to Cite

Mwathi, V. W., Makoti, V., & Mutua, J. (2024). Uhusiano wa Lugha na Tabaka: Uchanganuzi wa Riwaya za Kuli na Pendo la Karaha. Nairobi Journal of Humanities and Social Sciences, 8(1). https://doi.org/10.58256/qkmf2486

References

Adam, S. (1979). Kuli. Dar es Salaam: Longhorn Publishers.

Bernstein, B. (1971). Class, Codes and Control: Theoretical Studies Towards a Sociology of Language. New York: Routledge.

Bourdieu, P. (1986). The Forms of Capital. Handbook of Theory and Research for the Sociology of Education. New York: Greenwood Press.

Bourdieu, P. (1991). Language and Symbolic Power. Cambridge, Massachusetts: Harvard University Press

Cameron, D. (1995). Verbal Hygiene. New York: Routledge.

Coulmas, F. (2013) Sociolinguistics: The Study of Speakers’ Choices. United Kingdom: Cambridge University Press.

Habwe, J. (2014). Pendo la Karaha. Nairobi: Moran Publishers.

Labov, W. (1966). The Social Stratification of English in New York City. Washington, DC: Center for Applied Linguistics

Lippi-Green, R. (2012). English with an Accent: Language, Ideology, and Discrimination in the United States. New York: Routledge.

Luthans, F. (2019). Organizational Behavior: An Evidence-Based Approach. (13th Edition). New York: McGraw-Hill Education.

McGregor, W. (2009) Linguistics: An Introduction. Great Britain: Bloomsburry Publishing Plc

Odetola, O and Ademola, A. (1987). Sociology: An Introductory African Text. Hong Kong: Macmillan Publishers.

Robbins, P & Judge, A. (2019). Essentials of Organizational Behavior (14th Edition). New York: Pearson

Vivian, C & Newson, M. (2007). Chomsky’s Universal Grammar: An Introduction. Hoboken: Blackwell Publishing.

Wardhaugh, R. (1997). An Introduction to Sociolinguistics. Great Britain: Blackwell Publishers.