Muundo wa Virai vya Sentensi ya Kîîgembe katika Kuafikia Maendeleo Endelevu kwa Waigembe
Keywords:
Eksibaa, Kîîgembe, virai, vipashioAbstract
Lugha kama chombo cha mawasiliano ni kipengele cha muhimu katika uafikiaji wa maendeleo ya kila jamii. Lugha za kiasili ni muhimu katika mawasiliano kwani ni lugha ambazo hushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi kuafikia maendeleo endelevu.Wanataaluma wengi wa isimu wamezipoka lugha hizi za kiasili kwa kutozifanyia utafiti jambo ambalo ni hatari. Aidha, ili jamii yeyote kuimarika katika uchumi na maendeleo lazima watumie lugha yao ya kiasili ila si lugha za kigani. Hiki ndicho kiliwachochea watafiti kutafiti muundo wa sentensi ya Kîîgembe ili kuweza kutumika katika shughuli mbalimbali Kirai ni kipashio cha muundo chenye neno moja au zaidi lakini kisicho na muundo wa kikundi nomino na kikundi tenzi. Virai ni mojawapo ya vipashio vya sentensi ya Kîîgembe vinavyoshughulikiwa katika taaluma ya sintaksia. Makala hii inashughulikia muundo wa virai vya sentensi ya Kîîgembe kwa kufafanua kanuni zinazoongoza uunganishwaji wa virai kuundia sentensi ya Kîîgembe.Data ya sentensi 50 imetumika katika makala hii. Virai aina tano vilichanganuliwa na kuainisha miundo ya virai katika Kîîgembe na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo. Makala hii inachangia katika kuongeza maarifa ya kiutafiti kuhusu sentensi ya Kîîgembe, kutumika kwa lugha hii kwa kuchangia maendeleo endelevu na kuhifadhi maandishi yake.
References
Besha, R. M. (1994). Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dares salaam. Macmillan Aidan Ltd.
Chomsky, N. (1957). Syntactic Structures. The Hague: Mouton.
Chomsky, N. (1970). Aspect of the Theory of Syntax. Cambridge: MIT Press
Chomsky, N. (1986). Knowledge of Langauge, Its Nature, Origin and Age. New York: Praeger.
Cowper, E.(1992). A Concise Introduction to Syntactic Theory: The Government-Bindin Approach. Chicago: The University of Chicago Press
Jerono, P. (2003). Kishazi Huru Arifu cha Kiswahili: Mtazamo wa x-baa.(Tasnifu ya Uzamili haiyachapishwa) Chuo Kikuu Cha Nairobi.
Khamisi, A. A. (2011). Uchambuzi wa Kiswahili Fasaha: Sarufi na Lugha, Zanzibar: Kikuu cha Elimu Chukwani
Leffel, K. na Bouchard, D. (1991). Views on Phrase Structure Kluwer Academic Publishers, Dordrecht, The Netherlands
Massamba, na wenzake (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA). Sekondari na Vyuo, Dares-salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
Massamba, na wenzake (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dares Salaam. TUKI.
Matei, A. (2008) Sarufi Kamili ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix.
Mkude, J. J. D. (1983). Uchanganuzi wa Sentensi za Kiswahili: Dar es salaam: TUKI
Mukuthuria, M. (1997). Njeo katika Kitenzi cha Kitigania. Tasnifu ya Uzamili katika Kiswahili, [haijachapishwa] Chuo Kikuu cha Egerton.
Newmeyer, F. J. (1986). Linguistic Theory in America 7th Edition Orlando: Academic Press Inc. Chicago University Press. Radford, A. (1981). Transformational Syntax. Cambridge: Cambridge University Press.
Newmeyer, F. J. (1988). Transformational Grammar. Cambridge: Cambridge University Press
Rubanza, Y. I. (2003). Sarufi: Mtazamo wa Kimuundo, Dares salaam.Chuo Kikuu cha Huria cha Tanzania.
Wesana-Chomi, E. (2017). Kitangulizi cha Muundo Viambajengo wa Sentensi za Kiswahili. Dar es Salaam: Taasisi ya Taaluma za Kiswahili.
Downloads
Published
Issue
Section
License
This open-access article is distributed under a Creative Commons Attribution (CC-BY) 4.0 license.
You are free to: Share — copy and redistribute the material in any medium or format. Adapt — remix, transform, and build upon the material for any purpose, even commercially. The licensor cannot revoke these freedoms as long as you follow the license terms.
Under the following terms: Attribution — You must give appropriate credit, provide a link to the license, and indicate if changes were made. You may do so in any reasonable manner, but not in any way that suggests the licensor endorses you or your use.
No additional restrictions You may not apply legal terms or technological measures that legally restrict others from doing anything the license permits.